Raia wa Ethiopia wakamatwa Manyara wakielekea Afrika Kusini

0
47

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linawashikilia raia 17 wa Ethiopia wanaodaiwa kuingia nchini bila kibali wakielekea Afrika Kusini.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Lucas Mwakatundu amesema raia hao wamekamatwa Aprili 7, mwaka huu katika mtaa wa Maisaka, mjini Babati wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 VXR ambalo waling’oa baadhi ya viti ili waenee wote.

“Tunatarajia kuwakabidhi kwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua nyingine, ikiwemo kufikishwa mahakamani na kujibu shtaka linalowakabili,” amesema Kaimu Kamanda Mwakatundu.

Ameongeza kuwa bado hawajabaini mmiliki wa gari hilo lililokuwa na namba mbili (T723 BSF na STL 1964) ni nani, na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kumbaini mmiliki wa gari hilo.

Send this to a friend