Raia wa Kenya adukua mifumo ya Zimbabwe na kuiba bilioni 280

0
44

Mwanamke mmoja raia wa Kenya anakabiliwa na mashitaka ya ulaghai nchini Zimbabwe baada ya kudaiwa kuhusika katika udukuzi wa mifumo ya Mfuko wa Maendeleo ya Wafanyakazi wa Zimbabwe (ZIMDEF) na kuhamisha dola milioni 120 (TZS bilioni 280) kutoka kwenye akaunti ya benki ya wakala wa serikali.

Primrose Nyeri Mwangi (40) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Primkett Travel and Tours and Mafkett Trading, anadaiwa kushirikiana na watu wengine wawili kudukua mifumo ya data ya ZIMDEF ambapo walipata ‘codes’ za kuiba pesa kutoka kwenye akaunti za shirika hilo.

FBI inachunguza nyaraka za siri zilizopatikana katika ofisi ya Rais Bidden

Aidha, washitakiwa hao pia wanadaiwa kuhamisha fedha nyingine katika akaunti ya Atrier Engineering CBZ, Newplaces (Pvt) Limited akaunti ya NBS na akaunti ya Tavaka Holding NBS.

Gazeti la Herald limeripoti kuwa kosa hilo lilifichuliwa Desemba 28, 2022 na mtoa taarifa aliyetuma barua pepe kwa mlalamikaji kuwatahadharisha kuhusu miamala hiyo.

Mbali na hilo, Mwangi pia anakabiliwa na shitaka la ziada la kufanya biashara nchini Zimbabwe ilhali alikuwa nchini humo kwa visa ya kitalii.

Send this to a friend