Raia wa Tanzania akamatwa Msumbiji kwa tuhuma za ugaidi

0
112

Jeshi la Msumbiji limemkamata raia wa Tanzania ambaye anadaiwa ni kiongozi wa kikundi cha kigaidi katika Wilaya ya Nangade katika Jimbo la Cabo Delgado.

Kijana hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Ali, mwenye umri wa miaka 39 amekamatwa pamoja na watu wengine sita ambao wanahusishwa kuwa na mfungamano na kundi la kigaidi la Dola ya Kiislamu (Islamic State).

Afisa wa jeshi amesema kuwa Ali ni mmoja wa viongozi wa kikundi hicho ambao jukumu lao ni kutafuta wapiganaji wapya na kuratibu mashambulizi.

Kumekuwa na mfululizo wa mashambulio katika wilaya hiyo ambapo ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kuwa kumekuwa na mashambulio saba ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Shmabulio la mwisho lilitokea katika Kijiji cha Lamualamua siku ya Jumamosi ambalo lilipelekea vifo vya watu sita waliokuwa kwenye sherehe.

Send this to a friend