Raia/wasafiri kutoka Tanzania kuwekwa karantini siku 14 nchini Kenya

0
39

Serikali ya Kenya imefanya maboresho ya orodha ya nchi ambazo raia wake au wasafiri kutoka nchi hizo hawatawekwa karantini kwa siku 14 wakiingia nchini humo, ikiwa ni muendelezo wa hatua za kuhakikisha nchi inakuwa salama dhidi ya virusi vya corona.

Orodha hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya inajumuisha nchi 130 zikiwemo nchi mbalimbali za Afrika Mashariki lakini Tanzania haimo.

Hii ina maana kuwa raia au wasafiri watakaoingia Kenya kutoka Tanzania watalazimika kukaa karantini kwa siku 14 kuthibitisha kuwa hawana maambukizi ya virusi hivyo.

Agosti 1 mwaka huu Kenya ilitoa orodha ya nchi ambazo ndege zake zinaweza kuingia Kenya, lakini Tanzania haikuwemo. Hatua hiyo ilipelekea Tazania kuzuia ndege za Kenya kuingia nchini, mvutano ambapo baada ya muda mfupi ulipatiwa ufumbuzi.

Baadhi ya nchi za Afrika zilizomo katika orodha hiyo ni Namibia, Morocco, Ethiopia, Seychelles, Eritrea, Gambia, Mauritius, Tunisia, Misri, Libya, Botswana, Zimbabwe, Djibouti, Lesotho na Angola.

Nchi zisizo za Afrika ni Italia, Falme za Kiarabu, Singapore, Marekani (isipokuwa California, Florida na Texas) na Thailand.

Wasafiri wote watalazimika kuonesha cheti kinachothibitisha kuwa wamepimwa maambukizi ya virusi vya corona ndani ya saa 96 kabla ya safari.

Pia, msafiri hatotakiwa kuwa na joto linalozidi 37.5°C, au kuwa na kikohozi, tatizo la upumuaji na dalili nyingine za mafua.

Kenya ilifungua anga lake Agosti 1 mwaka huu baada ya kulifunga tangu Machi 2020 huku ikiruhusu ndege za mizigo na zile za dharura.

Hapa chini ni orodha kamili iliyotolewa ya nchi ambazo raia au wasafiri wake hawatowekwa karantini;

Send this to a friend