Rais aagiza 40% ya mapato ya halmashauri yaende kwenye maendeleo

0
57

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kutumia asilimia 40 ya mapato yanayokusanywa na halmashauri kuelekezwa katika shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo leo wakati akisalimiana na waanchi wa Chunya katika ziara yake iliyoanza jana mkoani humo, ambapo amesema mapato ya ndani yanayokusanywa mkoani Mbeya yanaweza kutekeleza shughuli nyingi za maendeleo ikiwemo ujenzi wa stendi ya Chunya.

“Pamoja na kwamba mmeomba Serikali tuweke jicho [ujenzi wa stendi, Chunya], tutaangalia juhudi zenu. Kama kweli mnataka stendi tutaona mnachofanya na sisi ndipo tutakapowaongezea. Lakini mkizubaa mnasubiri Serikali ilete, Serikali ina mambo mengi sana ya kufanya,”amesema.

Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa, Serikali inajitahidi kutekeleza ahadi zilizoahidiwa katika ilani ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara pamoja na ujenzi wa madarasa nchini.

“Halmashauri, MaDC kaeni vizuri, mwakani tunahitaji madarasa 8,000 kwa Tanzania nzima ya Sekondari mbali ya Primary [msingi]. Kwa hiyo karibu tutaanza kutimuana tena kwa ajili ya madarasa.”

Send this to a friend