Rais aelekeza gharama za sherehe ya Uhuru zikarabati miundombinu

0
80

Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa mwaka huu hakutakuwa na sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru (Desemba 9), badala yake fedha zilizokuwa zimetengwa kwa shughuli hiyo zitumike kukarabati miundombinu iliyoharibiwa wakati wa vurugu Oktoba 29.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na wananchi mkoani Dar es Salaam baada ya kukagua athari za vurugu hizo.

“Mheshimiwa Rais ameelekeza tarehe 09, hakutakuwa na sherehe za kuadhimisha hiyo Desemba 09. Na gharama ya fedha ambazo zingekuwa zitumike kwenye sherehe, ameelekeza ziende kutengeneza miundombinu hii iliyoharibika,” amesema.

Aidha, katika hotuba yake, Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulifungulia Kanisa la Ufufuo na Uzima, na taasisi nyingine za kidini, na iziweke chini ya uangalizi kwa miezi sita.

Ameielekeza wizara hiyo kutofungia kanisa au msikiti pindi kiongozi anapokosea kwani inaleta madhara kwa wananchi. “Akikosea Sheikh, usiadhibiwe msikiti na akikosea Askofu, wasinyimwe waumini kufanya ibada.”

Send this to a friend