Rais afanya uteuzi mpya, Mchechu ateuliwa Hazina, Makame NHC

0
21

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Nehemia Mchechu kuwa Msajili wa Hazina. Kabla ya uteuzi huo Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mchechu anachukua nafasi ya Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Wakati huo huo, Rais Samia amemteua Hamad Abdallah kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kabla ya uteuzi huo, Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

Aidha, Rais Samia amemteua Mussa Makame kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Kabla ya uteuzi huo, Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na pia ni Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania.

Makame anachukua nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.