
Rais Samia Suluhu amempa zawadi ya shilingi milioni mbili bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi maarufu Dullah Mbabe licha ya kupigwa kwa pointi katika pambano la Knockout ya Mama lililofanyika Februari 28, 2025.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa amesema Rais Samia ametoa zawadi hiyo kutokana na mchango wa bondia huyo kwenye ngumi huku mabondia wengine wakipewa zawadi ya shilingi milioni moja kila mmoja.
“Dulla Mama kasema nikupatie shilingi milioni mbili, anajua umepoteza lakini kwa mchango wako mkubwa kwenye boxing, endelea ku-inspire vijana, waendelee kucheza wawatie moyo vijana wengine,” amesema Msigwa.
Kwa upande wake bondia Dullah Mbabe amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa zawadi kumpa zawadi hiyo.