Rais amuagiza Waziri Mkuu kuongeza saa 24 za uokoaji Kariakoo

0
5

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo Novemba 16, mwaka huu.

Akizungumza kwa njia ya simu, Rais Samia amesema anatambua kuwa utaratibu wa uokoaji ni saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo, lakini anaamini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kutenda miujiza na kuweza kuwanusuru wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo.

“Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la uokoaji, na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai,” amesema Rais.

Ameongeza, “Kwa vikosi vyetu na wananchi wote wanaopambana kuokoa maisha ya ndugu zetu katika zoezi hilo, ninaomba ufikishe salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na ninawathamini sana. Wameonesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu sana. Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania zetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu.”

Send this to a friend