Rais amwondoa Maharage TTCL, avunja bodi ya REA 

0
39

Rais Samia Suluhu amemteua Maharage Chande kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huo, Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na sasa anachukua nafasi ya Macrice Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imeeleza kuwa Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo Septemba 23, mwaka huu akisubiri kupangiwa kazi nyingine.

Aidha, Rais Samia amemteua John Ulanga kuwa Balozi. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Pia, Rais amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kumteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Gedion Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi REA.

Send this to a friend