Rais aridhia wafanyabiashara wapya kutolipa kodi kwa muda wa hadi mwaka mmoja

0
43

Rais Samia Suluhu Hassan ameruhusu wafanyabiashara wanaoanza biashara kutolipa kodi kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08,2023 yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kondoa.

“Rais ametoa kibali, wale wanaoanza biashara kufanya biashara miezi sita hadi mwaka mmoja ndipo waanze kulipa kodi,” amesema.

Amesema hatua hiyo inaonesha jinsi gani Rais Samia Suluhu anavyowajali wananchi na kutoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa katika kuleta maendeleo.

Aidha, amewataka wananchi kuachana na mikopo umiza kwa kuwa imekuwa ikiwaumiza kutokana na kuwa na riba kubwa.

Mbowe: Serikali na CCM ziliwasaidia wabunge 19, ni uhuni usiovumilika

“Halmashauri zimekuwa zikitoa mikopo ya asilimia nne, wananchi mwende mkope huko. Pia Rais Samia ametoa fedha kwenye Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ambapo mikopo hutolewa kwa riba ya asilimia tisa,” ameeleza

Send this to a friend