Rais asisitiza mashirika kuzalisha zaidi ili kuleta mageuzi ya kiuchumi

0
14

Rais Samia Suluhu Hassan ameyataka mashirika ya umma na taasisi za ndani kufanya kazi kwa bidi na kuzalisha zaidi ili uchumi wa Tanzania uendelee kukua na si kurudi nyuma.

Akizungumza leo wakati akipokea Gawio na Michango kutoka kwa mashirika na Taasisi za Umma Ikuku Dar es Salaam, amesema kwa sasa Tanzania imekua kiuchumi na inaelekea katika uchumi wa kati hivyo mageuzi yanapaswa kuendelea ili kuhimili nafasi hiyo pasipo kutetereka.

“Mnapoingia uchumi wa kati baadhi ya mambo haya tunayoyapata sasa hivi yanakatwa, mkopo kama ule tuliopata juzi [nchini Korea] Dola bilioni 2.5, lipa kwa miaka 40, entrace rate ni 0.01 hutapata tena kwa sababu umeshajikongoja kiuchumi umeingia kwenye uchumi wa kati.

Sasa tusipojitahidi huku ndani, mashirika yetu yasipojitahidi kuzalisha huku ndani tuka export [kusafirisha bidhaa nje] sana, tukapata fedha, ile sifa ya kwenda uchumi wa kati itatutokea puani itabidi turudi tena kulekule na mimi sipo tayari,” amesema.

Aidha, amesema mageuzi yaliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam ya kukaribisha sekta binafsi yameleta faida kubwa kwa Serikali, ambapo ameeleza kuwa Serikali inatarajia kupata mafanikio makubwa zaidi katika bandari zote kubwa nchini.

Send this to a friend