Rais Dk Magufuli kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato

0
39

Rais Dk John Pombe Magufuli anatazindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato Julai 09 mwaka huu, ambapo pamoja na mambo mengine, atakabidhi vibali na hati kwa wawekezaji mbalimbali ili kuwekeza katika eneo hilo.

Hifadhi hiyo imepandishwa hadhi hivi karibuni kutoka lililokuwa Pori la Akiba la Burigi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangala amesema hayo wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari wanaokutana jijini Mwanza, ulioandaliwa na shirika la hifadhi za Taifa Tanapa, ukiwa na Kauli Mbiu ya Miaka 60 ya shirika hilo katika kuimarisha uhifadhi na kupanua wigo na fursa za Utalii kusini, Magharibi na Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania.

Dk Kigwangala akabainisha kuwa Uzinduzi wa Hifadhi hiyo mpya ya Taifa ya Burigi Chato, una nia ya dhati ya kufungua saketi ya Uhifadhi na Utalii Kaskazini-Magharibi badala ya ule wa kaskazini pekee uliozoeleka.

Amebainisha Sekta ya Utalii ina mchango mkubwa katika ukuaji wa pato la Taifa kutokana na kuingiza fedha nyingi za kigeni ikilinganishwa na sekta zingine, na kwa sasa sekta hiyo inachangia asilimia 17.6 kwenye pato la taifa.

Send this to a friend