Rais Dkt. Mwinyi aanza kubana matumizi kwa kutoteua Naibu Mawaziri

0
33

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza Baraza la Mawaziri lenye wizara 15, akiwa amefanya mabadiliko ya baadhi ya wizara na kuhamishia wizara nyingine chini ya ofisi yake.

Dkt. Mwinyi amesema kuwa hatoteua Naibu Mawaziri kama ilivyozoeleka hadi pale itakapomlazimu, kwani moja ya malengo yake ni kubana matumizi ya serikali.

Hapa chini ni orodha ya mawaziri 13 walioteuliwa leo;

  1. Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji – Mudrik Ramadhan Soraga
  2. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Talawa za Mikoa na Vikosi vya SMZ- Masoud Ali Mohammed
  3. Ofisi ya Rais Katiba, Sheria na Utumishi na Utawala Bora- Haroun Ali Suleiman
  4. Ofisi ya Rais Fedha na Mipango – Jamal Kassim Ali
  5. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Dkt. Khalid Salum Mohammed
  6. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo- Dkt. Soud Nahoda Hassan
  7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali- Simai Mohammed Said
  8. Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni na Michezo- Tabia Mwita Maulid
  9. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi- Riziki Pembe Juma
  10. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale- Leyla Mohammed Mussa
  11. Wizara Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi-Rahma Kassim Ali
  12. Wizara Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Abdallah Hussein Kombo
  13. Wizara ya Maji na Nishati- Suleiman Masoud Makame
  14. Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda- (Ipo wazi)
  15. Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Watoto- (Ipo wazi)

Akizungumzia uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye anatakiwa kutoka chama cha upinzani chenye kura zaidi ya asilimia 10 amesema;

“Tumewaandikia ACT Wazalendo walete jina la Makamu wa Kwanza wa Rais, lakini jina halijafika, hivyo nafasi tumeiacha wazi.”

Dkt. Mwinyi amesema wizara mbili alizoziacha wazi (Wizara ya Viwanda na Wizara ya Afya) ni kwa ajili ya ACT Wazalendo. Amesisitiza kuwa endapo watajiandikisha Baraza la Wawakilishi ndani ya muda wa kikatiba, atawateua.

Send this to a friend