Rais Dkt. Mwinyi afuta gwaride Sherehe ya Mapinduzi

0
52

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema hakutakuwepo na hafla ya gwaride la kilele cha sherehe za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo hufanyika Januari 12 kila mwaka.

Akizungumza na vyombo  mbalimbali vya habari leo Jumamosi Desemba 31, 2022, Dkt. Mwinyi amesema fedha zilizotakiwa kutumika kwenye kilele cha maadhimisho hayo zitakwenda kwenye miradi ya maendeleo sekta ya elimu.

“Huwa tunakuwa na gwaride kwenye uwanja wa Amaan, safari hii halitakuwepo, sababu kuu ni mbili; ya kwanza, tumeona kama serikali tujipange kuadhimisha jambo kubwa zaidi kwa mwaka ujao ambapo mapinduzi yetu yatatimiza miaka 60,” amesema.

Dkt.  Mwinyi ameeleza kuwa shule nyingi zinafunguliwa hivyo Serikali imelenga kutumia fedha hizo kununua vifaa vya kutosha katika shule mbalimbali.

Aidha, ametaja  kiasi kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya kilele cha maadhimisho hayo kuwa ni TZS milioni 450 ambazo zitaelekezwa  kwenye sekta hiyo ya elimu.

Send this to a friend