Rais Dkt. Mwinyi na Dkt. Kikwete watunukiwa tuzo Marekani

0
23

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete wamekabidhiwa Tuzo ya Rais (Presidential Award) ya Mwaka 2023 nchini Marekani kwa kutambua mchango wao katika sekta ya maji.

Tuzo hizo zimetolewa na Taasisi ya Global Water Changemakers kwa mara ya kwanza mwaka huu kwa wakuu wa nchi na Serikali sita waliopo madarakani na waliostaafu kwa kutambua mchango wao katika kuonesha dhamira ya kweli ya kusimamia na kuleta mabadiliko chanya katika kuendeleza sekta ya maji katika nchi wanazotoka na barani Afrika.

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masis katika kongamano linalohusu maji la Umoja wa Mataifa linaloendelea jijini New York, Marekani.

Viongozi wengine waliopokea tuzo hizo ni wenyeviti wenza wanne wa Jopo la Ngazi ya Juu la Kimataifa la Uwekezaji wa Maji kwa Afrika ambao ni Rais wa Senegal, Macky Sall, Rais wa Namibia, Rais Hage Geingob, Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte na Rais wa Zambia, Rais Hakainde Hichilema.

Send this to a friend