Rais Kagame aonya shughuli za kidini zinazotukuza umasikini

0
38

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amewaonya vijana dhidi ya kujihusisha na mila na desturi zinazoweza kuendeleza umaskini, ikiwa ni pamoja na zile zinazofanywa katika muktadha wa dini.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na zaidi ya vijana 2000 waliohudhuria maadhimisho ya miaka 10 ya mradi wa YouthConnect katika Ukumbi wa Mkutano wa Intare Conference Arena huko Rusororo.

Rais Kagame alikuwa akirejelea hija inayofanyika kila mwaka kwa siku tatu ambayo vijana wengi kutoka Magharibi mwa Rwanda hushiriki na wengine hutembea usiku na mchana kwa miguu bila kula chochote na kuhitimisha katika eneo la ‘Mlima wa Maombi’ unaojulikana kama Bikira Maria wa Maskini ulioko Parokia ya Crête Congo Nil, wilayani Rutsiro.

BRICS yaongeza wanachama wapya sita zikiwemo Ethiopia na Misri

“Kwa hiyo, mmefikia hatua ya kuabudu umaskini? Nilidhani unapoomba, unaomba vitu vinavyoweza kukusaidia kujitengenezea na kukutoa kwenye umaskini,” Kagame aliwahoji vijana.

Aliongeza kuwa “Endapo nitapata kusikia jambo kama hili tena, kwamba watu walikwenda kuabudu umaskini, nitapeleka malori na kuwakamata na kuwafunga gerezani, na kuwaachilia tu wakati fikra za umaskini zitakapowaondoka,

Kiongozi huyo aliwasihi vijana kukataa mila kama hiyo na waepuke tabia za kukata tamaa na kutokujiamini na badala yake wazingatie mambo yanayowanufaisha wao na nchi yao.

Send this to a friend