Rais Kagame kufanya ziara nchini Aprili 27 na 28

0
67

Rais wa Rwanda, Paul Kagame anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini kuanzia Aprili 27 hadi 28, mwaka huu ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo yao.

IMF yaidhinisha mkopo wa TZS bilioni 358 kwa Tanzania

Rais Kagame ataongozana na ujumbe wake na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Tanzania na Rwanda zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu ambapo nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo biashara na uwekezaji, nishati, uchukuzi, elimu na utamaduni.