Rais Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais

0
34

Rais wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Magufuli, amechukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kiongozi huyo amechukua fomu hiyo kuomba ridhaa ya chama ateuliwe kugombea tena, baada ya kuteuliwa mwaka 2015, ambapo awamu yake ya kwanza inaelekea kumalizika.

Rais amechukua fomu hiyo katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma na amekabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally.

Baada ya kuchukua fomu hiyo amesema kuwa anaanza zoezi la kutafuta wadhamini na ataanzia jijini Dodoma.

Send this to a friend