Rais Magufuli aeleza alivyomuonya mkurugenzi kabla ya kumtumbua leo

0
11

Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Revocatus Kuuli.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia tuhuma za kujitwalia ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na ubadhirifu wa fedha za maduhuli ya Serikali zinazomkabili Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Dkt. Magufuli ametangaza uamuzi huo aliposimama kuwasalimu wananchi wa Igunga wakati akiwa safarini. Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Phillemon Sengati kuteua mtumishi mwadilifu atakayekaimu nafasi hiyo mpaka hapo uteuzi wa mkurugenzi mwingine utakapofanyika.

Amesema pamoja na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, anazo taarifa nyingi za dosari za Bw. Kuuli, alishamuonya juu ya vitendo vyake vya kuwadhulumu wananchi wakiwemo wanawake na hivyo Serikali anayoiongoza haiwezi kumvumilia kiongozi wa namna hiyo.

Aidha, amewapongeza wananchi wa Tabora, Igunga na Nzega kwa kupata maji kutoka Ziwa Victoria na amewasihi kutumia maji hayo vizuri kwa manufaa yao.

Send this to a friend