Rais Magufuli aeleza makundi mitandaoni yanavyovujisha siri za serikali

0
23

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli amesema kuwa serikali inafanya kazi zake kwenye karatasi na sio kwenye makundi ya mitandao kama ambavyo baadhi ya watendaji wamekuwa wakifanya.

Dkt. Magufuli amesema hayo wakati akizungumza baada ya kiwaapisha mawaziri na naibu mawaziri Ikulu Chamwino leo ambapo amewataka viongozi hao na wengine kuangalia taarifa zinazotumwa kwenye makundi na kulinda maadili na usiri wa serikali.

“… ndani ya serikali sasa hivi kuna ugonjwa mmoja, hata mawasiliano yanatumwa kwenye group [kundi], barua nyingine ni za siri… Na ndiyo maana siri ndani ya serikali zinavuja…” amesema Dkt. Magufuli.

Amesema maendeleo ya teknolojia yaliyopo sasa ni mazuri lakini lazima watumishi wote waangalie ni maeneo gani pakuitumia.

“…. kwenye mambo ya serikali ni lazima mzingatie maadili ya viapo vyetu. Si kila kitu kinapelekwa kwenye magroup,” ameeleza Dkt. Magufuli akisisitiza usiri katika shughuli za serikali.

Aidha, kabla ya Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu alizungumza na kuwataka wote walioapishwa, wapya na wenyeji kufanya kazi kwa bidii.

Amesema kuwa uteuzi wao umezingatia taaluma, utendaji wao na tabia na hulka zao katika jamii, na hivyo wajua wao ni safu ya kuanzia na kwamba kuna wengine wengi nje ambao watachukua nafasi zao endapo hawatofanya kazi vizuri.

Katika hafla hiyo ya uapisho iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali, mawaziri 21 na naibu mawaziri 23 wameapishwa tayari kianza kutumika.

Send this to a friend