Rais Magufuli afanya mabadiliko wizara ya afya

0
49

Rais Dkt. Magufuli amemteua Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Mchembe alikuwa Msaidizi wa Rais katika masuala ya afya.

Wakati huo huo, Rais amemteua Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Chaula alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na amechukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Maria Sasabo ambaye amestaafu.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali (Chief Medical Officer).

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Abel Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na amechukua nafasi iliyoachwa na Prof. Mohamed Bakari Kambi ambaye amestaafu.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 22 Aprili, 2020.

Send this to a friend