Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara

0
36

Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Delphine Diocles Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

Dkt. Magere anachukua nafasi ya Bi. Theresia Mmbando ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Magere alikuwa Ofisi ya Rais akishughulikia masuala ya uchumi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dunstan Kyobya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mkoani Mtwara.

Kyobya anachukua nafasi ya Evod Mmanda aliyefariki Dunia tarehe 27 Aprili, 2020.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kyobya alikuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.
uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 06 Mei, 2020.

[Picha: Maktaba]

Send this to a friend