Rais Magufuli afanya uteuzi wa Wakurugenzi watatu

0
48

Rais Dkt. Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi 3 kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Bi. Anastazia Tutuba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Tutuba alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Mkoani Arusha na anachukua nafasi ya Bi. Anna-Claire Shija.

Pili, Rais Magufuli amemteua Bw. Saad Mutambule kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Mkoani Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mutambule alikuwa Afisa Mipango wa Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya na anachukua nafasi ya Bi. Alvera Ndabagoye ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Bw. Elias Amede Ng’wanidako kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Ng’wanidako alikuwa Mweka Hazina wa Jiji la Mbeya na anachukua nafasi ya Bw. James Kasusura ambaye amestaafu.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 04 Julai, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.

Send this to a friend