Rais Magufuli agawa pikipiki kwa maafisa tarafa

0
40

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli ametoa pikipiki 12 kwa Maafisa Tarafa mkoani Rukwa ili ziweze kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kiserikali katika kata wanazozihudumia.

Pikipiki hizo zimetolewa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa tarehe 04.06.2019 baada ya kufanya kikao kazi na Maafisa Tarafa wote nchini alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameshukuru rais kwa kutimiza ahadi hiyo huku akiwasisitiza maafisa hao kutumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kusimamia mapato, miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Wakati akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Maafisa Tarafa wenzake, Afisa Tarafa ya Kasanga, Andrew Ngindo baada ya kumshukuru Rais Magufuli, alimuomba mkuu wa mkoa kuona uwezekano wa kutengewa bajeti ya mafuta pamoja na matengezo kwa pikipiki hizo ili ziendelee kuwarahisishia utekelezaji wa majukumu yao. 

Send this to a friend