Rais Magufuli amrejesha kazini Mkurugenzi aliyesimamishwa kazi 2016

0
41

Rais Dk Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati kumrejesha kazini mara moja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio.

Katika agizo lake alilolitoa leo Julai 22, Rais ameitaka Wizara ya Nishati kumrejesha Dkt. Mataragio katika nafasi yake ya Mkurugenzi Mkuu wa TPDC ili aendelee na majukumu yake.

Dkt. Mataragio alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC tarehe 20 Agosti, 2016.

Kusimamishwa huko kazi kulitokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) ya mwaka 2015 iliyoeleza kuwa, TPDC ilikiuka taratibu za manunuzi ya umma kwa kuipa upendeleo kampuni ya Marekani kutafiti mafuta na gesi katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa Ziwa Tanganyika, Songosongo, Mandawa na Eyasi.

Send this to a friend