Rais Magufuli amteua Jaji Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili

0
14

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi (Jaji wa Mahakama ya Rufani) kuwa Kamishna wa Maadili.

Jaji Mwangesi ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu, Harold Nsekela kufariki dunia.

Uteuzi wa Jaji Mwangesi unaanza leo Disemba 23, 2020 na ataapishwa Disemba 24, 2020 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Send this to a friend