Rais Magufuli asema mipaka haitafungwa, watu wachape kazi

0
39

Rais Magufuli amesisitiza kuwa Serikali imeamua kutowazuia watu ndani ya nyumba zao wala kufunga mipaka kwa kutambua madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kutokana na kufanya hivyo ndani ya nchi na kwa nchi 8 ambazo zinategemea kupata huduma na bidhaa kupitia Tanzania hususani Bandari ya Dar es Salaam.

Rais amesema hilo alipoungana na waumini wa Kanisa Katoliki katika Parokia ya Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kusali ibada ya Ijumaa Kuu.

Amebainisha kuwa kutokana na madhara ya ugonjwa huo duniani, upo uwezekano wa kutokea upungufu wa chakula, hivyo ametoa wito kwa Watanzania kuzalisha chakula cha kutosha na pia amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi kila mahali walipo huku wakichukua tahadhari za kutoambukizwa kama wanavyoelekezwa na wataalamu.

Pia, amewataka Watanzania wote kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili aiepushe dunia na janga la ugonjwa wa Corona.

Send this to a friend