Rais Magufuli atengua agizo la wizara kuhusu mafunzo ya ualimu

0
23

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli amefuta agizo lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwa Rais serikali imefuta mafunzo ya ualimu wa shule za msingi na awali kwa ngazi ya cheti na kuwa mafunzo yataanzia ngazi ya stashahada.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo alipopiga simu kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Waalimu Duniani ambalo linafanyika jijini Dodoma.

“Kuna tangazo moja linazunguka zunguka, mlipuuze hilo tangazo ni la kipumbavu,” amesema Dkt. Magufuli.

Amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na walimu kwani ilianza nao na itamaliza nao.

Maadhimisho ya siku ya walimu yalianza mwaka 1994 yakiwa na lengo ya kuangazia mazingira na changamoto zinazowakabili walimu, kuzitatua ili kutengeneza kizazi bora.

Send this to a friend