Rais Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Tawala Wilaya kwa tuhuma za kuchukua wake za watu

0
55

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) ya Kisarawe, Mtela Mwampamba kutokana na makosa ya kinidhamu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Kibamba-Kisarawe mkoani Pwani, Rais ameeleza kutoridhishwa na uteuzi wa kiongozi huyo ambaye amekuwa akituhumiwa kuchukua wake za watu.

Aidha, kufuatia utenguzi huo, akiwa mkutanoni hapo Rais Magufuli amemteua Afisa Tawala, Mwanana Msumi kuwa DAS, baada ya mtendaji huyo kupendekezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.

Rais Magufuli ameendelea kuwasisitiza wasaidizi wake aliowateua kuhakikisha wanafanya kazi kwa maslahi ya wananchi.

Send this to a friend