Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD

0
32

Rais Tanzania Dkt Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Dkt. Gabriel Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).

Taarifa iliyotolewa na Murugenzi Mkuu wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa, uteuzi wa Dkt Mhidize unaanza mara moja.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Lugalo jijini Dar es salaam.

Brigedia Jenerali Dkt Mhidize anachukua nafasi ya Laurean Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Send this to a friend