Rais Magufuli ateua Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam

0
46

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Julai, 2020 amefanya uteuzi wa viongozi wa Mikoa na Wilaya kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Aboubakar Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kunenge alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bw. Paul Christian Makonda.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mkirikiti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na anachukua nafasi ya Bw. Alexander Pastory Mnyeti.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Paulo Mshimo Makanza kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Makanza alikuwa Afisa Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na anachukua nafasi ya Bw. Aboubakar Kunenge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Nne, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Seleman Serera kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Serera alikuwa Afisa Mwandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu na anachukua nafasi ya Bw. Deo Ndejembi.
Tano, Mhe. Rais Magufuli amemteua Ssgt. Mayeka Simon Mayeka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Kabla ya uteuzi huo, Ssgt. Mayeka alikuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na anachukua nafasi ya Bi. MarryPrisca Makundi.

Sita, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali Patrick Norbert Songea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Kanali Songea alikuwa Afisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na anachukua nafasi ya Bw. Tumaini Magesa.

Saba, Mhe. Rais Magufuli amemteua Alhaji Rajab Kundya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Kabla ya uteuzi huo, Alhaji Kundya alikuwa Afisa katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu na anachukua nafasi ya Bw. Kippi Warioba.

Nane, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Kashushura Rwiza kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Rwiza alikuwa Afisa Mipango katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora na anachukua nafasi ya Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya.

Tisa, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Gharib Lingo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Lingo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Kumi, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Frank Fabian Chonya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Chonya alikuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi na anachukua nafasi ya Bw. Andrea Godfrey Chezue.

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kept (Mst) George Huruma Mkuchika, kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Bw. Juvenile Jaka Mwambi kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara.

Bw. Juvenile Jaka Mwambi anachukua nafasi ya Bw. Benaya Liuka Kapinga.

Pili, amemteua Bw. Mashaka Boniface Mgeta kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
Bw. Mgeta anachukua nafasi ya Bw. Boniface Maiga aliyefariki dunia hivi karibuni.

Tatu, amemteua Bi. Johari Khamis Athuman kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Bi. Johari Khamis Athuman alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Bw. Aboubakar Asenga.

Nne, amemteua Bw. Ayoub Amir Perro kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Perro alikuwa Afisa katika Ofisi ya Upelelezi ya Polisi Mkoa wa Kigoma na anachukua nafasi ya Twaha A. Mpembenwe.

Send this to a friend