Rais Magufuli ateua Mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi watano

0
46

Rais Dkt Magufuli amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri 5 kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Lauteri Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kanoni alikuwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Songwe na anachukua nafasi ya Bw. Ally Mohammed Kasinge.

Pili, amemteua Bw. Bashir Paul Mhoja kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mhoja alikuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita na anachukua nafasi ya Bw. Robert Mgendi Masunya.

Tatu, amemteua Bw. Ramadhan Salmin Possi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Possi alikuwa Afisa Mipango katika Jiji la Tanga Mkoani Tanga na anachukua nafasi ya Bi. Amina Kiwanuka ambaye amestaafu.

Nne, amemteua Bw. Baraka Michael Zikatimu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Zikatimu alikuwa Afisa Mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mkoani Tanga na anachukua nafasi ya Bi. Margareth Jonathan Nakainga ambaye amestaafu.

Tano, amemteua Bw. John John Nchimbi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Nchimbi alikuwa Afisa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoani Morogoro.

Sita, amemteua Bw. Emmanuel Matinyi Johnson kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Emmanuel Matinyi Johnson alikuwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 07 Julai, 2020.

Send this to a friend