Rais Magufuli ateua viongozi wapya ngazi ya wilaya

0
45

Rais Dkt. Magufuli amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya mmoja na Mkurugenzi Mtendaji mmoja kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera John Bulimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.

Kabla ya uteuzi huo, ACP Bulimba alikuwa Kamanda wa Kikosi cha Polisi TAZARA na anachukua nafasi Godfrey Ngupula.

Pili, amemteua Solomon Isack Shati kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Shati alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi na anachukua nafasi ya Bryceson Paul Kibasa.

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kept (Mst) George Huruma Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Tanzania, amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya mbili, kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Omary Mwanga kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi. Mwanga anachukua nafasi ya Husna Juma Sekiboko.

Pili, amemteua Saitoti Zelothe Stephen kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Saitoti Zelothe Stephen alikuwa Afisa Tarafa Wilayani Mbulu katika Mkoa wa Manyara na anachukua nafasi ya Hassan M. Mkwawa.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 09 Julai, 2020.