Rais Magufuli ateua wakurugenzi wapya watano

0
45

Rais Dkt Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wengine 5 kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Bw. Duncan Golden Thebas kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Duncan Golden Thebas alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma na anachukua nafasi ya Bw. Mussa Chimae.

Pili, amemteua Bw. Mwailafu Thomas Edwin kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba Mkoani Mtwara.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwailafu Thomas Edwin alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida na anachukua nafasi ya Bw. Oscar Antony Ng’itu.

Tatu, amemteua Bi. Erica Epaphras Yegella kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Erica Epaphras Yegella alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya na anachukua nafasi ya Bw. Omari Juma Kipanga.

Nne, amemteua Bw. Hassan Njama Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Hassan Njama Hassan alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji wa Mtwara Mkoani Mtwara na anachukua nafasi ya Bw. Florent L. Kayombo.

Tano, amemteua Bw. Kanyala Malima Mahinda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kanyala Malima Mahinda alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani na anachukua nafasi ya Bw. Francis K. Ndulane.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 04 Julai, 2020 na wateule wote wanat

Send this to a friend