Rais Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa 3,900

0
17

Katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano, Mhe. Rais Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3,973 ambapo kati yake wafungwa 3,717 wamesamehewa vifungo vyao, na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.

Rais ametoa msamaha huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka Aprili 26.

Amesema ana matumaini kuwa wafungwa hao wamejifunza na watajirekebisha ili waungane na jamii katika kulitumikia Taifa wakiwa raia wema wanaozingatia sheria na taratibu.

Amewataka Watanzania wote kutumia siku ya kesho (26 Aprili, 2020) kuutafakari Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa Corona.

Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona (Covid-19) ikiwemo kujiepusha na mikusanyiko na safari zisizo za lazima

Send this to a friend