Rais Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kutanguliza maslahi ya nchi mbele na kuhakikisha amani inaendelea ili wananchi waendelee na shughuli zao na serikali itekeleza miradi ya maendeleo
Dkt. Magufuli amesema hayo leo alipokutana na kufanha mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad waliomtembelea nyumbani kwake Chato mkoani Geita.
“Tunatakiwa Watanzania tutangulize maslahi ya mataifa yetu kwanza. Maadui zetu wangefurahi sana kuona tunagombana na Zanzibar inachafuka lakini wameshindwa kwa sababu viongozi nyie hamkuwa na mawazo ya kuvunja umoja wa kitaifa.”
Aidha, amewashukuru sana Dkt. Mwinyi na Maalim Seif na kisema “mmefanya lililo jema, mmewafanyia mema Wazanzibar na sasa mambo ya ubaguzi huyu mpemba huyu muunguja hayatakuwepo tena kama yatakuwepo ninyi mkahubiri huo umoja.”
Kwa upande mwingine amesema mwanga wa maendeleo umeanza kuonekana visiwani humo na kuahidi kuendelea kushirikiana na viongozi hao.