Rais Magufuli awataka wanasiasa kutotumia matusi na kejeli kwenye uchaguzi

0
41

Vyama vya Siasa nchini vimehakikishiwa uwepo wa uhuru na haki sawa kwa vyama vyote vitakavyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Rais Dkt. Magufuli wakati akitoa hotuba ya kuvunja Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo jijini Dodoma.

Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu kama ilivyokuwa kwa chaguzi zingine zilizopita unakuwa wa uhuru na haki.

“Tutasimamia uhuru na haki wa vyama vyote, na hii ndiyo Demokrasia ya kweli, kwa sababu hiyo navisihi vyama vya siasa na wanasiasa kujianda vizuri kushiriki kwenye uchaguzi huu”, ameisitiza Rais Magufuli.

Aidha, ametoa wito kwa vyama vya siasa kutoa fursa ya kutosha kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kushiriki uchaguzi huu katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametoa rai kwa watakaogombea na kushiriki uchaguzi huo kujiepusha na matumizi ya lugha za matusi na kejeli na badala yake wafanye kampeni kwa kushindanisha hoja huku wakimtegemea Mungu zaidi.

Send this to a friend