Rais Magufuli: Corona imeondolewa nchini kwa nguvu za Mungu

0
44

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufulia amesema kuwa ugonjwa wa homa ya mapafu (Covid-19) unaosababishwa na virusi vya corona umeondolewa nchini kwa nguvu za Mwenyenzi Mungu.

Ameyasema hayo alipojumuika na waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Chamwino mkoani Dodoma katika Misa Takatifu ya Sikukuu ya Utatu Mtakatifu.

Aidha, amewashukuru viongozi wa dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania na janga la corona.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa makini dhidi ya mbinu zozote zinazoweza kufanywa kuwaambukiza ugonjwa huo ama magonjwa mengine, huku wakimshukuru na kumtumaini Mwenyezi Mungu aliye muweza wa yote.

Akiwa kanisani hapo Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha shilingi 17,229,000/- (ikiwemo shilingi Milioni 10 aliyochangia yeye mwenyewe) na mifuko 76 ya saruji, na ametaka upanuzi wa kanisa hilo uanze kesho (Juni 8, 2020).

Send this to a friend