Rais Magufuli: Mwanangu aliugua corona, akajifukiza, amepona

0
41

Rais DKt John Pombe Magufulia amesema kuwa mwanae wa kumzaa alipata maambukizi ya virusi vya corona, na sasa ni mzima wa afya.

Rais Magufuli amesema hilo alipokuwa akitoa salamu kwa Watanzani leo wakati aliposhirikia ibada Jumapili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato Mkoani Geita.

“Mimi ninapozungumza hapa, nina mtoto wangu alipata Corona, mtoto wa kuzaa mimi. Amejifungia kwenye chumba akaanza kujitibu, akajifukizia, akanywa malimao na tangawizi, amepona, yupo mzima sasa anapiga pushup,” amesema Rais Magufuli

Amesisitiza kuwa isionekane kwamba anachukua hatua fulani kwa sababu ugonjwa huo haujampata, na kuongeza kuwa ni kweli watu watakaugua baada ya ugonjwa kusambaa lakini utakwisha.

Katika hatua nyingine, amesema endapo hali ya wagonjwa wa corona itaendelea kupungua kama ilivyo sasa, atafungua vyuo na kuruhusu shughuli za michezo.

Send this to a friend