Rais Magufuli na Rais Kenyatta wafikia muafaka hali ya mipakani

0
29

Rais wa Tanzania, John Magufulia amesema kuwa amezungumza na mwenzake, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuhusu suala la mipakani mwa nchi hizo mbili, na wamekubaliana kutafuta ufumbuzi wa pamoja.

Rais Magufuli amesema hilo leo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Singida, ambapo amewataka wakuu wa mikoa iliyopo mpakani mwa Tanzania na Kenya kutotatua matatizo yao kwa jazba.

“Viongozi waliopo katika mipaka inayopakana na nchi ya Kenya na Tanzania, wasitatue matatizo yao kwa jazba, waweke Utanzania na Ukenya mbele,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, ametoa agizo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na wakuu wa mikoa inayopakana na Kenya (Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Mara) kukutana wiki hii na wenzao wa Kenya kujadili namna ya kupata ufumbuzi wa migogoro ya mipakani.

Amesisitiza kuwa virusi vya corona havikuanzia Afrika, hiyo isifike mahali Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikashindwa kufanya biashara kwa sababu ya corona.

Send this to a friend