Rais Magufuli: Tutatengeneza ajira milioni 8

0
52

Serikali imeahidi kutengeneza ajira takribani milioni 8 katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ikiwa ni mkakati wa kupunguza umasikini miongoni mwa Watanzania na kukuza uchumi.

Hayo yamesema na Rais Dkt. John Magufuli wakati akitoa hotuba yake ya kufungua rasmi Bunge la 12 ambayo imetoa muelekeo wa serikali kwa kutaja maeneo mbalimbali ambayo itajikita kuyafanyia kazi kwa miaka mitano ijayo.

“Tumepanga kuendeleza jitihada za kukuza uchumi. Tutahakikisha ukuaji wa uchumi unanufaisha wananchi kwa kuinua vipato vyao, kupunguza umasikini na tatizo la ajira. Tunalengo la kukuza uchumi kwa angalau 8% kwa mwaka na kutengeneza ajira zipatazo milioni 8.”

Aidha, ikiwa ni sehemu ya makati wa kupunguza umasikini na kukuza uchumi, Rais Magufuli amesema watawawezesha “wananchi wetu kiuchumi kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba au yenye riba nafuu ikiwemo mikopo ya halmashauri zetu pamoja na kupitia mifuko na programu mbalimbali zilizoanzishwa na serikali.”

Pia ameahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya watumishi wote ili yaendane na hali halisi ya maisha ya Watanzania.

Send this to a friend