Rais Magufuli: Wengine mnaweza msichukue fomu muamue Magufuli amepita

0
43

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufulia amesema kuwa wagombea wa vyama vingine wanaweza kuamua kutokuchukua fomu za kugombea Urais wa Tanzania, badala yake waamue kuwa yeye (Rais Magufuli) amepita.

Kiongozi huyo ambaye pia ni mgombe wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema hilo mapema leo asubuhi wakati akizundua jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma ambapo ndipo fomu za wagombea zitakapotolewa.

“Ninawashukuru sana wenyeviti wenzangu, hili ndilo jengo letu, tutakuja kuchukulia fomu hapa, lakini mnaweza mkaamua siku hiyo mkaacha kuchukua mkasema tu Magufuli umepita ili fedha hizi zikatumike kwenye shughuli nyingine za taifa letu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kutotumia nguvu katika mchakato wote wa uchaguzi, lakini pia amewasihi wanasiasa nao kutokufanya mambo ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kusapelekea vyombo hivyo kutumia nguvu.

Pia, amependekeza ndani ya jengo hilo la ghorofa nane, vyama mbalimbali vya siasa vipewe ofisi za kufanya shughuli zao kwa sababu wote ni Watanzania.

Send this to a friend