Rais mpya wa Malawi ateua ndugu kuwa mawaziri

0
29

Rais mpya wa Malawi amekosolewa vikali kufuatia kuteua watu ambao ni ndugu na watu wake wa karibu katika baraza lake jipya la mawaziri.

Katika baraza hilo Rais Dkt. Lazarus Chakwera amemteua aliyekuwa mgombea mwenza katika uchaguzi wa 2019, Sasik Mia kuwa Waziri wa Usafiri na mke wake, Abida Mia ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi.

Kenny Kandodo ameteuliwa kuwa Waziri wa Kazi wakati dada yake Khumbize Kandodo ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya nchini humo.

Miongoni na hao, mfanyabiashara Gospel Kazako ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari na shemeji yake Agnes Nkusa ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Awali Mwanasheria Modercai Msiska alikataa nafasi aliyokuwa ameteuliwa ya Waziri wa Sheria na kusema kuwa kitendo hicho kingeonesha amepewa zawadi kwa kumuwakilisha kiongozi huyo mahakamani wakati wa kesi ya kupinga ushindi wa Rais Peter Mutharika.

Watu wengi wamemkosoa Rais Chakwera kwa kurudia aliyokuwa akimkosoa mtangulizi wake kuyatenda ya kuteua wanandugu au watu wake wa karibu kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.

Aidha, watu wengine wanamkosa kiongozi huyo ambapo wamesema kuwa baraza lake hilo limejumuisha 70% ya watu kutoka kanda ya kati eneo ambalo chama chake kina nguvu.

Send this to a friend