Rais Mstaafu, Dkt. Shein ateuliwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe

0
41

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi tatu, ambapo kwanza amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Dkt. Shein anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas A. Samatta ambaye anamaliza muda wake.

Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Dkt. Mwakyembe anachukua nafasi ya Bi. Mariam Joy Mwaffisi ambaye amemaliza muda wake.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudentia Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Bi. Kabaka anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Novemba 24, 2020.

Send this to a friend