Mahakama nchini Comoro imemhukumu kifungo cha maisha jela Rais Mstaafu nchi hiyo, Ahmed Abdallah Sambi ambaye amepatikana na hatia ya kuuza hati za kusafiria kwa watu wasio na uraia waishio katika mataifa ya Ghuba.
Sambi (64) amehukumiwa leo Novemba 28, 2022 na Mahakama ya Usalama ya Jimbo, chombo maalum cha mahakama ambacho maamuzi yake hayawezi kukatiwa rufaa.
Majambazi wasimamisha mahubiri kanisani na kuwaibia waumini
Waendesha mashtaka nchini Comoro walikuwa wakitaka Rais huyo wa zamani ahukumiwe kifungo cha maisha jela kwa ubadhirifu wa mamilioni ya dola, huku hukumu yake ikitoka bila ya yeye kuwepo mahakamani baada ya kukataa kuhudhuria kesi.
Rais huyo ambaye ni mpinzani mkubwa wa Rais wa sasa, Azali Assoumani aliongoza nchi hiyo tangu 2006 hadi 2011 na kupitisha sheria mwaka 2008 inayoruhusu uuzaji wa hati za kusafiria kwa gharama za juu