
El expresidente de Perú Alejandro Toledo POLITICA EL COMERCIO / ZUMA PRESS / CONTACTOPHOTO
Mahakama nchini Peru imemhukumu Rais wa zamani, Alejandro Toledo (74) kifungo cha miaka 13 na miezi minne jela kwa utakatisha fedha wakati akiwa madarakani.
Toledo ambaye aliwahi kuwa Rais kati ya mwaka 2001 na 2006, alipatikana na hatia ya kutumia rushwa kutoka kampuni ya ujenzi ya Brazil Odebrecht (sasa ikijulikana kama Novonor) kununua nyumba na ofisi za kifahari jijini Lima.
Hukumu hiyo ni ya pili, baada ya mwaka 2024 kupatikana na hatia ya kupokea rushwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 na miezi 6 jela, ambapo alipokea kiasi cha dola milioni 35 [TZS bilioni 87.7] kutoka kampuni hiyo ili kuwapa zabuni za miradi ya umma.
Toledo atatumikia hukumu zote kwa pamoja katika gereza maalumu ambako pia wanashikiliwa marais wa zamani, Ollanta Humala na Pedro Castillo.








