Rais Mteule wa Nigeria aenda mapumziko Ulaya

0
26

Rais Mteule wa Nigeria, Bola Tinubu amesafiri hadi nchini Ufaransa na Uingereza ili kupumzika na kupanga mpango wa mpito kabla ya kuapishwa kwake Mei 29 mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake siku ya Jumatano, Tunde Rahman, amesema Rais huyo mteule aliondoka nchini Nigeria siku ya Jumanne na anatarajiwa kuadhimisha Hijja nchini Saudi Arabia.

Kenya: Viongozi 6 hatarini kufungwa kwa kuratibu maandamano

“Rais Mteule aliamua kupumzika baada ya kampeni na msimu wa uchaguzi wenye shughuli nyingi kupumzika Paris na London, kujiandaa kwenda Saudi Arabia kwa Umrah (Hajj Ndogo) na mfungo wa Ramadhan unaoanza Alhamisi,” amesema.

Tinubu anakabiliwa na vita vya kisheria kuhusu ushindi wake katika uchaguzi wa Urais wa mwezi uliopita nchini Nigeria.

Send this to a friend