Rais Museveni aungwa mkono kugombea urais mwaka 2026

0
68

Makamu wa Rais, Maj Jessica Alupo, Waziri wa Mambo ya Ndani Meja Jenerali Kahinda Otafiire, na Waziri wa Ulinzi Vincent Sempijja ni miongoni mwa viongozi wa Uganda ambao wametia saini barua ya kumuunga mkono Rais Yoweri Museveni kugombea tena urais mwaka 2026.

Tukio hilo limefanyika wakati viongozi hao walipohudhuria sherehe ya Siku ya vijana ya Wilaya ya Mitooma nchini Uganda zilizofanyika chini ya kaulimbiu “Kukuza Uwezo na Nafasi ya Vijana katika Maendeleo ya Taifa.”

Waziri wa Sheria nchini humo, Norbert Mao amewaambia vijana huko Mitooma kuwa Rais amempa jukumu la kuandaa makubaliano ya mpito nchini Uganda kuanzia 2031 ambao utakuwa katika awamu tatu; makubaliano, kuridhia na utekelezaji wa yale yatakayokubaliwa.

Rais Museveni (78) ameongoza Uganda tangu mwaka 1986. Mnamo 2026, atakuwa na umri wa miaka 82.

Send this to a friend