Rais Museveni kuikabidhi serikali shule aliyoijenga wilayani Chato

0
36

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewasili nchini Tanzania leo Jumamosi Novemba 27, 2021 kwa ziara ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaa.

Akiwa katika ziara ya siku tatu nchini Tanzania, Rais Museveni atafanya mambo mbalimbali ambayo ni:

1. Yeye na mwenyeji wake watashiriki ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda ambalo pamoja na masuala mengine litajikita katika sekta ya mafuta na gesi.

2. Atatembelea Bandari ya Dar es Salaam na kukagua mradi unaoendelea wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) katika eneo la Stesheni Kuu.

3. Rais Museveni atafanya ziara wilayani Chato, mkoani Geita ambapo ataikabidhi Serikali ya Tanzania shule ya msingi iliyojengwa kwa ufadhili wake wilayani humo.

4. Ataitembelea familia ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Magufuli.

Mara baada ya shughuli hiyo, Rais Museveni atahitimisha ziara yake ya siku tatu nchini na kuagana na mwenyeji wake kisha kurejea nchini kwake Uganda.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Museveni kufanya ziara nchni mwaka huu, ambapo Mei 2021 alifika nchini na kushuhudia utawaji saini wa mikataba ya utelekeza wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Send this to a friend